......ilikuwa ni Franklin Bulls walioanza kumiliki mpira, lakini moja kwa moja Payton Hughes anafanikiwa kupora mpira na kuwapa Kendry Rams nafasi ya kushambulia kwa haraka. Rams wanajaribu kutumia fursa hio kushambulia kwa haraka lakini cha kushangaza kijana mdogo Tom Isaac ambaye hakuhusika kabisa na kwenye ulinzi, tayari alikuwa mbele kabisa ya uwanja upande mwingine wa eneo la kushambulia. Rams wanaonekana kucheza sana eneo la ulinzi huku wakiumuacha Isaac eneo la kushambulia makusudi ili apate nafasi ya kushambulia kwa haraka, hii ilikuwa mbinu ya ajabu sana ya kumuacha acheze upande moja tu. Rams wanajaribu kupiga pasi ndefu ya haraka inayofanana na sara ya salama maria lakini Bulls wanazuia shambulio hilo kwa kurudi haraka. Tom anajaribu kupiga kwenye nafasi nzuri ili wapate walau pointi tatu lakini anakosa, hata hivyo Rams wanapata nafasi ya mpira uliorudishwa, Martin anatumia nafasi ya pili vizuri wanafunga na kupata pointi. Inashangaza kuona kitu kama hiki kwenye mpira wa kikapu, kutoka kwa Rams kilikuwa ni kitu cha ajabu....